Hili ndilo gari ambalo alilokuwa akitumia Waziri  wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, na kuopata nalo ajali  juzi akiwa safarini kutoka Dodoma kuelekea jijini Mwanza kikazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Antony Luta, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Kata ya Nyandekwa wilayani Igunga mkoani hapa, ikihusisha gari lenye namba za usajiri STK 8780.

Luta alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi la Green Star lenye namba za usajili T939 TRA ambalo lilikuwa likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam, alipokuwa akijaribu kulipita lori katika mlima huku gari la waziri huyo likitokea upande wa pili.

Dereva wa waziri aliyetambulika kwa jina la Saidi Komando, alijaribu kulikwepa basi hilo, lakini akashindwa na hivyo gari likapinduka mara tatu na kusababisha watu watatu akiwemo Waziri Fenella kujeruhiwa.

Kamanda Luta alisema mara baada ya ajali hiyo, waziri huyo na majeruhi wengine walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega kwa matibabu na kwamba mipango ya kuwahamishia katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma zinafanywa.
Dereva wa basi la Green Star, Daniel Chawa (32), alikamatwa baadaye na polisi wilayani Igunga, baada ya kuwa amekimbia awali na hivyo atafikishwa mahakamani.

Hali ya Dkt Mukangara inaendelea vizuri. Akiongea na Globu ya Jamii sasa hivi yupo Dar es salaam alikorejea jana jioni na kupata matibabu zaidi katika kitengo cha mifupa cha MOI hospitali ya Muhimbili. Amesema baada ya kuchukuliwa vipimo vyote ameonakana hana madhara mwilini zaidi ya michubuko na  majeraha mengine madogo. Anashukuru kwamba wote walikuwa wamefunga mikanda na kwamba air-bags za gari hilo zimeokoa maisha yao.

Amewashukuru sana madaktari wa Nzega na wa kitengo cha dharura cha Muhimbili ambao walimhudumia pamoja na wa hospitali ya Regency alikopatiwa vipimo vya CT-Scan. Pia anawashukuru watanzania wote waliomuombea nafuu, wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2012

    mchuma wa maana ndio ukaona limefunguka airbag gari nzima sio ile nyingine iliyemuuwa yule mbunge hata airbag haina sijui ilikuwa ya mchina

    pole sana mh. waziri

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2012

    CT SCAN REGENT HOSPITAL BADALA YA HOSPITAL YA TAIFA?YALE YALE

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuokoa dada yetu Fenella. We mdau wa 06:23:00 PM kwani hujui madaktari wa Muhimbili wako katika mgomo, japo hao madaktari wanafiki "walimaliza kwa muda" mgomo wao kumtibu muuaji so-called "Dr" Ulimboka jana pale MOI?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    Mchangiaji wa pili, hamna hospitali inaitwa Regent. Kuna hospitali inaitwa Regency. Kama hujui, uliza. Ndiyo maana Waswahili wanasema kuuliza si ujinga........

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2012

    CT scan ya Muhimbili iliharibika miezikadhaa iliyopita.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...