Taswira hizi zilinaswa na kamera ya Globu ya Jamii hivi karibuni wilayani  Ngorongoro, moja kati wilaya tano zinazounda mkoa wa Arusha nchini. Wilaya hii inapakana na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini, Wilaya ya Monduli kwa upande wa Mashariki, Wilaya ya Karatu kwa upande wa Kusini na mkoa wa Mara kwa upande wa Magharibi.
Eneo maarufu na linalojulikana sana ulimwenguni la Ngorongoro kreta liko katika wilaya hii. Pia mlima wenye volkano hai ujulikanao kama Oldoinyo Le Ngai upo katika wilaya hii. Kwa maana hii wilaya nzima ya Ngorongoro ni eneo lililohifadhiwa. Kabila kuu katika wilaya ya Ngorongoro ni Wamasai. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro ilihesabiwa kuwa 129,776

 Morani

Vijana 
Kinamama
 Mkeka wa nguvu kuelekea Ngorongoro
 Eneo maarufu na linalojulikana sana ulimwenguni la Ngorongoro kreta
Mlima wenye volkano hai ujulikanao kama Oldoinyo Le Ngai

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. hii nchi wee acha tu, sasa hao wanawake uwezekano upo wa kuolewa na kabila jingine na kuhamia Dar ?

    ReplyDelete
  2. Che GuevaraAugust 07, 2012

    Sura za hao akina dada sio wamasai bali ni wambulu a.k.a WAIRAQ

    ReplyDelete
  3. Si mchezo.Picha ya juu kabisa wa kwanza kutoka kulia...macho ya mtego hayo!!

    David V

    ReplyDelete
  4. Ah, mavazi asilia na miwani ya jua! Imenikumbusha Is It Possible? kwa wale ma-bookworm wenzangu...

    ReplyDelete
  5. Warembo wa Mujini kumekucha!

    Enhee wa mujini mukae mkao wa kiupinzani maana na wenzenu mademu wa msituni wameanza kuujua uzuri kwa kuanza kuvaa mawani.

    Kazi kwenu!

    ReplyDelete
  6. Nikirudi Bongo jambo moja ambalo ni lazim nilifanye ni kutembelea sehemu hizi. Ngoja nikuambie kisa kilichonisibu.Tulikuwa kwenye hafla baada ya harusi ya jamaa huko London, vijana kama wanne hivi wakanizunguka walipoambiwa kuwa miye natoka Tanzania, wakaanza kuzungumza na kuisifu nchi, na matembezi yao ya Ngorongoro,aib,mie nimezaliwa Moshi, lakini hiyo Ngorongoro naisikia tu.

    ReplyDelete
  7. Ankal picha nzuri sana.
    Picha zote hapo unaweza ukatengeneza pot card nzuri sana.
    Hasa m-tz alie nje anafurahia sana mantdar hizi asilia.

    Tanzania yetu ni nzuri.

    Eti uamsho ndo wanasema HAWAUTAKI.

    MDAU ZNZ

    ReplyDelete
  8. Hahahahaha mdau hapo juu umenikumbusha mbali sana Is It Possible? sijui kama siku hizi bado vitabu hivyo vinasomwa mashuleni, na kumbukuka na kile The River Between

    ReplyDelete
  9. Yaani kuna mdau hapo made my day! alivyosema kama kuna uwezekano wa kuoa na kumwamishia Dar! ushaona vijana wa kimasai walivyo na misuli nguvu za kutosha wamepikwa wamepikika.. wewe mdau wa Dar softiiii hujui hata kupambana.. utapata nafasi kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...