Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran ya Dubai, Dr. Asghar Fashad. Katika mazungumzon hayo, Mhe. Mjenga alimuomba Dr asghar kuangalia uwezekano wa kuwa na makubaliano kati ya hospitali yake na Ubalozi Mdogo kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa Watanzania kwa gharama nafuu ukilinganisha na gharama zake za sasa.

Baada ya mazungumzo na mashauriano ya muda wa saa moja, Uongozi wa Juu wa Hospitali, ulikubali ombi la Mhe. Mjenga la kupunguza gharama za matibabu kwa Watanzania kwa asilimia 40 (40%). Mwanzo, Uongozi ulipendekeza asilimia 20, ambayo Mhe. Mjenga aliwaeleza kuwa bado ilikuwa ni punguzo dogo na bado ingekuwa ni mzigo mkubwa kwa Watanzania. Hatmaye, ndio maafikiano hayo yakafikiwa ya asilimia 40.

Mpango wa huu utajumuisha Watanzania wote waishiyo UAE na wale wanaoishi nje ya UAE ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi Tanzania. Hospital ya Irani ni moja ya hospitali zenye huduma za hali ya juu kwa hapa Dubai na UAE kwa ujumla.

Uongozi wa Hospitali umekubali kuanza kutoa Vitambulisho Maalum kwa ajili ya Watanzania wote kuanzia Jumapili tarehe 1 Septemba. Mkataba wa Makubaliano haya utatiwa saini Jumatatu tarehe 2 Septemba.

Aidha, Mhe. Mjenga, amemuomba Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hii, kuangalia uwezekano wa kujenga Hospitali kubwa yenye hadhi kama hii, nchini Tanzania. Kimsingi, Mkurugenzi Mkuu amekubali ombi hili, na ameahidi kumuomba Rais wa Hospitali kufanya ziara nchini Tanzania mwezi ujao ili kuona na uongozi husika na kuanza mazungumzo ya kuanzisha Hospitali kama hiyo. Ameeleza kuwa Tanzania na Iran na nchi marafiki wa siku nyingi, na hivyo Iran inafarijika sana kuwa karibu na Tanzania kimahusiano.
Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Iran ya Dubai, Dr. Asghar Fashad pamoja na ujumbe wake wakati alipowa
Mhe. Omar Mjenga akiwa akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Dk. Asghar Fashad.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Anaonekana kuwa na akili ujuzi talent wa interprenuership afaa kuwa waziri.

    By Al Mahruqi

    ReplyDelete
  2. Mmmh, huyu nae afunguliwe tu ukurasa maalum.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...